Lugha Unayopendelea:

Saidia Maneno

Kama unapenda kile ambacho Maneno inafanya na unataka kutusaidia, tunapendekeza yafuatayo.
  • Toa mchango wa hisani
    - Vifaa
    Tunashirikiana na wanablogu wa Afrika, eneo ambalo ubadilishanaji taarifa huwezeshwa kwa teknolojia ya kubebeka (kuhamahama). Ikiwa una simu za mkononi zenye suhula za kuandikia (kama vile Blackberry) ambazo wewe au kampuni yako hamzitumii tena, tutafurahi kuzipokea kama mchango wa hisani na kuzisambaza kwa wanablogu hawa.
    $ USD
    - Fedha
    Sisi ni asasi isiyo ya faida iliyo na usajili kamili kupitia kifungu cha 501(c)3. Bajeti yetu ya uendeshaji inategemea michango ya hisani na misaada pekee. Endapo ungependa kututumia mchango wako wa hisani ambao pia utakatwa kodi, tafadhali jaza fomu iliyo mkono wa kulia. Kwa michango mikubwa ya hisani, misaada na zawadi tafadhali wasiliana nasi kupitia kiunganisho kilicho hapa chini. Tunathamini kujali kwako kwa kusaidia Maneno ipate kuendelea kutoa huduma na kupaaza sauti za Kiafrika.
     
    Endapo ungependa kuwasiliana nasi kuhusu yoyote kati ya hayo hapo juu, basi wasiliana nasi kupitia wasiliana nasi.
  • Jiunge kwenye Jumuiya
    Hata kama hufanyi shughuli za blogu kwenye Maneno, joining inakuunganisha kwenye jumuiya na kumwonyesha kila mwanajumuiya wewe ni nani. Inakuwezesha pia kutafsiri makala unazozipenda.
  • Beji
    Tembelea ukurasa wetu wa Eneza Ujumbe ili kuchukua namba ya siri ya beji utakayoiweka kwenye mtandao wako ili watu wengi zaidi wafahamu kuhusu Maneno.
  • Utumiaji Blogu
    Kama tayari una blogu yako, basi andika kuhusu Maneno. Pia unaweza kuiunganisha na makala unazoona zina mambo ya kuvutia. Kwa kufanya hivyo utakuwa ukiitangaza Maneno kwa hadhira pana zaidi, jambo ambalo ni moja ya malengo yetu.
  • Mabaraza ya Mtandaoni
    Kama una anwani ya Baraza la Mtandaoni katika eneo lenu barcamp.org, basi endesha mjadala kuhusu Maneno. Tunaweza kukupa orodha ya mada za kuzungumza, kama ukipenda. Tunaweza pia kukupa taarifa kuhusu Mabaraza ya Mtandaoni ya Afrika yaliyowahi kuwepo na pia miongozo juu ya namna ya kuyaendesha.
  • Tafsiri
    Moja ya vipengele vyetu vikuu katika Maneno ni maneno. Kama unaweza kutafsiri tovuti hiyo kwenye lugha nyingine mpya, utakuwa umetoa msaada mkubwa sana kwa tovuti hiyo. Ikiwa wewe unazungumza lugha nyingi, basi unaweza pia kutafsiri makala mbalimbali katika lugha nyingine ili ziwafikie watu wengi zaidi. Ili kufanya kazi hiyo, huhitaji kuwa na blogu, lakini itakuwa ni lazima ujisajili kwanza.