Lugha zinazotumiwa
Inakadiriwa kuwa kuna lugha zipatazo 2,000 zinazozungumzwa barani Afrika. Moja ya malengo makuu ya Maneno ni kutengeneza wavuti ambao unaweza kupatikana katika lugha nyingi kadiri inavyowezekana. Kwa sasa wavuti huu unasomeka katika lugha hizi: Bamanankan, English, Español, Français, Fulfulde, isiZulu, Kiswahili, Lingala, Português.Ongeza Lugha Yako
Maneno inategemea watu miongoni mwa jamii ili kutafsiri wavuti huu. Tunawahamasisha wale wote walio weledi wa lugha yoyote izungumzwayo Kusini wa Jangwa la Sahara kuwasiliana nasi contact us ili kutoa msaada kwa utaalamu wao wa lugha. Tafadhali usikatishwe tamaa hata kama lugha yako haina wazungumzaji wengi. Sisi bado tungependa kuwa nayo katika orodha yetu!Kutengeneza fasiri ni jambo rahisi. Mara tutakapopata mawasiliano kutoka kwako, tutakutumia faili kuu la msingi. Katika faili hilo, utaingiza maneno ya lugha yako kushika nafasi ya yale ya lugha tuliyokutumia, kisha unatutumia. Ukipenda, tutakupa shukrani zetu kupitia ukurasa huu na katika blogu yetu kwa kazi yako.
Wachangiaji
Bamanankan
Kazi yenye changamoto nyingi ya kutafsiri Maneno kwenda kwenye ki-Bambara ilifanywa na Boukary Konate wa nchini Mali. Yeye pia huandika makala zake kwenye Maneno kupitia Fasokan. Boukary ni mwalimu wa lugha za Kiingereza na Kifaransa jijini Bamako.

English, Español
Tafsiri hizi zilitengenezwa na Maneno. Endapo utakuta dosari yoyote au jambo ambalo linaweza kuelezwa vizuri zaidi, basi tafadhali wasiliana nasi kupitia contact us.

Français
Tafsiri hii ilikamilishwa na Claire Ulrich. Yeye ni mhariri wa Global Voices in French na pia ni mwandishi wa habari na mfasiri anayeishi Parisi.

Fulfulde
Oumar Bah ni mwenye asili ya Guinea, kwa sasa anaishi Austria. Ana shahada ya uzamiri katika lugha na sosholojia. Anazungumza na kuandika katika lahaja mbalimbali za Kifula. Yeye pia ni mwandishi wa kamusi ya Kifaransa-Kifula, ambayo inapatikana mtandaoni, na sasa anatafuta mchapishaji wa kuichapisha.

Kiswahili
Kazi nzuri ya tafsiri ya wavuti huu ilifanywa na Deogratias Simba anayeishi Dar es Salaam, Tanzania. Yeye ni mhariri kwa taaluma na mfasiri, ambapo amesaidia sana Maneno.

Lingala
Tafsiri ya Manemo katika Kilingala imefanywana Smalto Kabuya. Yeye ni mwanasheria anayeishi na kufanya kazi nchini Kenya. Vilevile yeye ni mfasiri wa Global Voices katika Kifaransa.

Português
Wavuti huu kwa sasa unatafsiriwa katika Kireno cha Brazili na watu kutoka Portuguese Global Voices.