Lugha Unayopendelea:

Utangulizi

Kwa Kiswahili, 'maneno' humaanisha 'maneno (matamshi vyenye kuleta maana)'.
"Maneno" ndiyo kiini muhimu katika Mtandao huu wa Maneno; tovuti iliyoanza kama kitu kidogo na hatimaye kukua na kuwa jukwaa la kuendeshea blogu na mawasiliano ili kukidhi mahitaji ya wanablogu na waandishi katika ukanda ulio chini ya Jangwa la Sahara.

    Lakini, kuna haja gani ya kuanzisha mfumo mwingine wa kublogu wakati tayari ipo mingi? Katika jumla yote ya watumiaji wa intaneti, ni 1% tu ndiyo wanaotoka barani Afrika, na katika asilimia hiyo, ni wachache tu ndiyo wanablogu. Mtandao wa Maneno unalenga kutoa nafasi kwa yale ambayo mitandao mingine huchukulia kama vitu vya kipuuzi, kisha kuyabadili hayo na kuyafanya yawe msingi wa mfumo madhubuti wa ufikishaji ujumbe chini ya Jangwa la Sahara.

    Kwanza imejengwa katika muundo mwepesi uliobuniwa na kutumiwa na waanzilishi, Maneno ilianzishwa mwaka 2008. Muundo huo unawasaidia hata wale ambao hupata mawimbi madogo au yanayosumbua ya intaneti ili waweze kutumia mfumo ambao ni mwepesi na wa moja kwa moja katika utendaji. Pamoja na kuwa na kasi nzuri katika ufungukaji wake, Maneno pia ni mfumo ambao una kila suhula ya kuwawezesha watumiaji kuwa na fursa mbalimbali za kwao kwa kadiri ya mahitaji yao, huku wakiandika pasipo kubanwa na chochote kadiri wanavyoona inafaa.

    Katika bara lenye lugha zaidi ya 2,000, suala la mawasiliano kutoka lugha moja kwenda nyingine mara nyingi huwa halipewi uzito hivyo kusahauliwa. Maneno ni mfumo ambao matoleo ya makala yaliyo katika lugha mbalimbali huwekwa pamoja kiasi cha kuruhusu mtu kuyatafuta kwa urahisi. Viunganisho vyake vikuu pia vimetafsiriwa katika lugha nyingi kadiri inavyowezekana ili kuondoa vikwazo vya lugha kama ambavyo tunashuhudia vikikua katika mtandao wa Lugha za KiAnglo (Mwelekeo wa Kiingereza).

twitter.com/maneno
facebook.com/maneno